Brandkidigitali Academy

Brandkidigitali Academy — Jifunze Digital Skills kwa Kiswahili Tanzania

Jukwaa Bora kujifunza Digital Skills — Brandkidigitali Academy Tanzania
Pata Kozi Zenye Soko la Ajira Tanzania — Brandkidigitali Academy Tanzania
Jiunge na Team ya Wataalamu Tanzania — Brandkidigitali Academy Tanzania

Jukwaa Bora kujifunza Digital Skills

Soko la ajira linahitaji vijana wabunifu pamoja na wataalamu wenye ujuzi unaoweza kutatua changamoto katika makampuni au biashara.

Wekeza Kwenye Ujuzi Wako wa Kidijitali

Kupitia mafunzo yetu ya vitendo, tunakupa maarifa sahihi na ya wakati sahihi yatakayokutengenezea fursa za kiuchumi kupitia ulimwengu wa kidijitali.

Chagua Skills Sahihi

Pata mafunzo ya vitendo katika Graphic Design, Video Editing, Social Media Management na Digital Marketing.

Pata Vyeti vya Uthibitisho

Maliza kozi zako na upate cheti kinachotambulika, kikuzae nafasi za ajira na ushindani sokoni.

Jifunze kwa Wataalam

Tunatoa usimamizi kutoka Beginner hadi Expert, tunakupa uzoefu wa majukumu halisi ya kazi.

Brand Kidigitali

Jukwaa hili limeanzishwa rasmi ikiwa na shauku kubwa ya kuboresha mfumo wa elimu ya vitendo kwa vijana nchini Tanzania. Dhamira yetu kuu ni kuziba pengo lililopo kati ya elimu ya darasani na soko halisi la ajira.

Tunatoa usimamizi kwa wanafunzi wanaotaka kubobea katika Graphic Design, Video Editing, Social Media Management, na Digital Marketing katika level kubwa ya ushindani wa soko la Tanzania.

Soma zaidi
Wanafunzi wa Brandkidigitali Academy

Jifunze Ujuzi Wenye Soko

Chagua kozi inayokufaa na uanze safari yako ya kujifunza

Hakuna matokeo

Hakuna kozi au vitabu vilivyopatikana kwa sasa.

Featured Courses

Siku zote katika kujifunza ujuzi wa kidijitali hakikisha unachagua kozi sahihi, njia sahihi ili kupata matokeo bora kwa muda sahihi.

Browse All Courses

Hakuna kozi kwa sasa.

Takwimu Zetu

Ukuaji wa Jukwaa Letu

Namna ambavyo jukwaa letu limeweza kubadilisha mtazamo wa vijana katika kujenga uchumi katika soko la mtandao na kuhakikisha wanatengeneza ajira binafsi na hata kuajiriwa.

0+

Wanafunzi

0+

Jumuiya

0+

Kozi Zilizopo

0+

Vyeti Vilivyotolewa

Jinsi Mafunzo Yanavyoendeshwa

Huu ndio utaratibu rahisi wa kupata mafunzo Brandkidigitali Academy.

Kujifunza kwa Video

Mwanafunzi anaanza kwa kujenga msingi thabiti kupitia Recorded Videos zilizokamilika pamoja na vitabu vya muongozo kwa lugha ya kiswahili. Hatua hii inampa uhuru wa kujisomea mahali popote na muda wowote unaomfaa kabla ya kuingia darasani.

Mazoezi ya Vitendo

Mafunzo haya yanatumia mbinu kamili (Action-Based Learning Approach), ambapo kila hatua ya masomo inaambatana na mazoezi ya vitendo (assignments). Mbinu hii haikupi tu nadharia, bali inakutaka utumie ujuzi papo kwa papo ili kujenga uzoefu wa kazi halisi za sokoni, ukijengewa uwezo na utayari kuajiriwa.

Msaada wa Wakufunzi

Wanafunzi wote wanaojiunga na mafunzo wanaunganishwa na Group la Whatsap. Mfumo huu unakuunganisha moja kwa moja na wakufunzi waliobobea kwa ajili ya kupata msaada wa haraka wa changamoto zako, huku ukishirikiana na wanafunzi wenzako jambo linaloongeza hamasa, kasi ya kujifunza, na mtandao (networking) wa kitaalamu.

Cheti na Portfolio

Mafunzo haya yanatumia mbinu ya "Kujenga Matokeo Yanayoonekana" (Outcome-Based Learning Approach), ambapo baada ya kukamilisha masomo na miradi yote ya vitendo, utapatiwa cheti rasmi cha kuhitimisha pamoja na portfolio thabiti ya kazi zako. Mfumo huu haukupi tu cheti, bali unakupa ushahidi kamili unaokuwezesha kujiamini wakati wa kuomba kazi.